15 Januari,2026 DC MBOGWE ATOA ELIMU KWA WACHIMBAJI WADOGO BUKANDWE
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Sakina Jumanne Mohamed, amekutana na wachimbaji wadogo waliopo Kata ya Bukandwe, eneo maarufu la Kanegere kwa Mchungaji, kwa lengo la kutoa elimu kuhusu shughuli za uchimbaji na ushirikiano na wawekezaji.
Akizungumza katika mkutano huo, DC Sakina amewahimiza wachimbaji wadogo kuzingatia sheria, taratibu na usalama kazini ili shughuli zao ziwe endelevu na zenye tija.
Nao Wachimbaji wamepongeza jitihada za Serikali na kuahidi kushirikiana katika kuendeleza sekta ya madini kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.